Fomu ya Kujiunga na Chuo cha VETA Arusha 2026

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hii hapa Fomu ya Kujiunga na Chuo cha VETA Arusha 2026 Taarifa Muhimu za Kuripoti – Muhula wa Kwanza 2026.

Bonyeza hapa kupakua fomu ya chuo cha veta Arusha PDF

Soma zaidi:

Mwanzo wa Muhula wa Mafunzo 2026

Mafunzo kwa Muhula wa Kwanza mwaka 2026 yataanza rasmi Jumatatu tarehe 13 Januari, 2026.

Mwanafunzi anatakiwa kuripoti chuoni ndani ya wiki mbili (2) kuanzia tarehe ya kufungua chuo. Endapo mwanafunzi hataripoti ndani ya muda huo, nafasi yake itapewa Mtanzania mwingine.

Muda wa mwisho wa kuripoti: Sio zaidi ya saa 10:00 alasiri.

Muda na Ngazi za Mafunzo

Mafunzo yamepangwa kufanyika kwa hatua tatu kama ifuatavyo:

  • Hatua ya Kwanza (Level I)
  • Hatua ya Pili (Level II)
  • Hatua ya Tatu na ya Mwisho (Level III)

Sifa na Nyaraka za Kuripoti

Mwanafunzi anatakiwa kuja na:

  • Cheti halisi (Original) cha Darasa la Saba au Kidato cha Nne au result slip
  • Nakala moja (Photocopy) ya cheti hicho

Baada ya kuthibitishwa na Dawati la Kujiandikisha, cheti halisi kitarudishwa kwa mwanafunzi na nakala kubaki chuoni kwa kumbukumbu.

Kumbuka: Leaving Certificate au Copy hazikubaliki.

Usalama Chuoni

Mwanafunzi anatakiwa kujinunulia Safety Boots zenye sifa zifuatazo:

  • Steel toe cap
  • Oil resistant sole

Wanafunzi wa fani ya Ushonaji hawahusiki.
Kwa ufafanuzi zaidi, fika Ofisi ya Mkuu wa Mafunzo Chuoni.

5. Mahitaji Muhimu ya Mwanafunzi

Kila mwanafunzi anatakiwa kununua vifaa vifuatavyo kwa matumizi binafsi akiwa chuoni:

  • Mashati mawili meupe (mikono mifupi – tetroni)
  • Suruali 2 rangi ya blue (zinapatikana chuoni)
  • Jozi 1 ya viatu vyeusi vya ngozi
  • Mathematical set, kalamu na penseli
  • Daftari 8 aina ya counter book (4 quire)
  • Sweta moja ya bluu, mavazi ya heshima na vifaa vya usafi binafsi
  • Overall/Overcoat rangi ya blue (vinapatikana chuoni)
  • Bima ya Afya NHIF (LAZIMA)
  • Godoro (wanafunzi wa bweni) – mita 2.5
  • Ream 1 ya karatasi za photocopy
  • Jembe, mfagio mgumu, mfagio laini, rubber squeezer
  • Blanketi, mashuka 2 rangi ya blue, neti ya mbu
  • Sahani, ndoo ya kuogea/kufulia, kikombe na kijiko

Ada ya Mafunzo – Muhula wa Kwanza 2026

Jedwali la Kwanza: Ada na Gharama Nyingine

Aina ya MalipoKutwa (TZS)Bweni (TZS)
Ada ya Mafunzo30,00060,000
Nembo ya VETA5,0005,000
Tahadhari20,00020,000
Kitambulisho5,0005,000
Michezo10,00010,000
Mahafali25,00025,000
Serikali ya Wanafunzi5,0005,000
Bima ya Afya NHIF50,40050,400
Jumla Kuu150,400180,400

Malipo yote yatafanywa kupitia Control Number utakayopewa chuoni.

Gharama za Mahitaji Yanayopatikana Chuoni

Mzazi/Mlezi anapaswa kuja na fedha taslimu siku ya kuripoti.

Mahitaji ya Ziada

MahitajiIdadiGharama (TZS)
T-shirt115,000
Overall135,000
Overcoat (Electronics & ICT)130,000
Suruali250,000
Jumla Kuu95,000 – 100,000

Utaratibu wa Kulipa Ada

  • Ada italipwa kwa awamu mbili
    • Awamu ya kwanza: Januari 2026
    • Awamu ya pili: Julai 2026 (Muhula wa Pili)
  • Malipo yote yatafanyika kwa Control Number ya Serikali utakayopewa na Mhasibu wa Chuo.

Ada za Mtihani (CBA)

Wanafunzi watakaofikia viwango vya ufaulu wataruhusiwa kufanya Mtihani wa Taifa wa Competence Based Assessment (CBA).

Kiasi cha ada ya mtihani kitatangazwa wakati wa likizo ndefu Juni/Julai 2026.

Bima ya Afya (NHIF)

Kila mwanafunzi anatakiwa kuwa na Bima ya Afya ya NHIF.

Mwanafunzi hatapokelewa chuoni bila kuwa na bima, hata kama ana bima ya nyumbani.

Utaratibu wa Kupokelewa Chuoni

Ni wanafunzi waliotimiza masharti yafuatayo pekee ndio watakaopokelewa:

  • Kulipa ada kamili
  • Kuwa na vifaa vyote vilivyotajwa
  • Kuwa na bima ya afya NHIF

Baada ya uhakiki, mwanafunzi atapewa Kibali cha Usajili na kupokelewa rasmi katika fani na bweni.