Hii hapa fomu na Jinsi ya Kujiunga na Chuo cha VETA Buhigwe 2026: Ada, Mahitaji na Sheria Muhimu
Kujiunga na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA Buhigwe) ni fursa muhimu kwa vijana wanaotaka kupata ujuzi wa vitendo unaohitajika kwenye soko la ajira. Makala hii inaeleza muda wa mafunzo, tarehe ya kuripoti, ada, mahitaji ya kujiunga na sheria za chuo kwa mwaka 2026 kwa ufupi na kwa kueleweka.
Bonyeza hapa kupakua fomu ya veta chuo cha Buhigwe PDF
Soma zaidi:
Mahitaji ya Jumla kwa Wanachuo Wote (VETA)
Kila mwanachuo anatakiwa kufika chuoni akiwa ametimiza masharti yote ya mahitaji, ada na taratibu zilizoainishwa hapa chini. Taarifa hizi ni muhimu kwa wanachuo wa kutwa na wa bweni.
Mahitaji ya Lazima kwa Wanachuo Wote
Kila mwanachuo anatakiwa kuwa na vifaa vifuatavyo kwa matumizi ya masomo na maisha ya kila siku chuoni:
- Mashati mawili meupe (mikono mifupi)
- Jozi moja ya viatu vyeusi vya ngozi vyenye visigino vifupi
- Viatu vya usalama (Safety Boots)
- Vifaa vya hesabu (mathematical set)
- Daftari 7 kubwa (counter book)
- Nguo za michezo (T-shirt na bukta rangi ya bluu) pamoja na raba
- Sweta moja la rangi ya bluu
- Ream moja ya karatasi A4 (NOPA au Mondi Rotatrim) itakayokabidhiwa kwa msajili siku ya kuripoti
- Wasichana waje na fyekeo moja
- Wavulana waje na jembe moja lenye mpini
Vifaa hivi vitakabidhiwa kwa msajili mara mwanafunzi anaporipoti chuoni.
Gharama za Mwanafunzi wa Kutwa (Day Scholar)
| Na | Mahitaji | Idadi | Kiasi (TSh) | Jumla (TSh) |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Ada ya mafunzo (mwaka mmoja) | 1 | 60,000 | 60,000 |
| 2 | Nembo | 2 | 3,000 | 6,000 |
| 3 | Fulana (T-shirt) | 1 | 15,000 | 15,000 |
| 4 | Kitambulisho | 1 | 10,000 | 10,000 |
| 5 | Suruali mbili | 2 | 20,000 | 40,000 |
| 6 | Fedha za tahadhari | 1 | 10,000 | 10,000 |
| 7 | Overcoat/Overall | 1 | 30,000 | 30,000 |
| 8 | Ufugaji wa samaki, kuku na ng’ombe | 1 | 35,000 | 35,000 |
| 9 | Mahafali | 1 | 30,000 | 30,000 |
| 10 | Picha (passport size) | – | 5,000 | 5,000 |
| Jumla Kuu | 241,000 |
Gharama za Mwanafunzi wa Bweni (Boarding Scholar)
| Na | Mahitaji | Idadi | Kiasi (TSh) | Jumla (TSh) |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Ada ya mafunzo (mwaka mmoja) | 1 | 120,000 | 120,000 |
| 2 | Nembo | 2 | 3,000 | 6,000 |
| 3 | Fulana (T-shirt) | 1 | 15,000 | 15,000 |
| 4 | Kitambulisho | 1 | 10,000 | 10,000 |
| 5 | Suruali mbili | 2 | 20,000 | 40,000 |
| 6 | Fedha za tahadhari | 1 | 10,000 | 10,000 |
| 7 | Overcoat/Overall | 1 | 30,000 | 30,000 |
| 8 | Ufugaji wa samaki, kuku na ng’ombe | 1 | 35,000 | 35,000 |
| 9 | Mahafali | 1 | 30,000 | 30,000 |
| 10 | Picha (passport size) | – | 5,000 | 5,000 |
| Jumla Kuu | 301,000 |
Utaratibu wa Malipo
- Malipo yote yafanyike kupitia mfumo wa serikali (GePG)
- Control number itapatikana katika ofisi ya VETA husika
- Jina kamili la mwanafunzi liandikwe kwenye slip ya benki
- Slip ya malipo ikabidhiwe kwa msajili mara tu mwanafunzi anaporipoti
- Mwanachuo wa bweni anatakiwa kuwa na kadi ya bima ya afya iliyo hai
- Mahitaji yatatolewa mara baada ya malipo kukamilika
Mahitaji ya Ziada kwa Wanachuo wa Bweni
Mwanafunzi wa bweni anatakiwa kuja na mahitaji yafuatayo binafsi:
- Mto
- Shuka
- Blanketi
- Chandarua
- Bakuli, sahani, kikombe na kijiko
- Ndoo au beseni la kuogea
- Ndala za kuogea
- Vifaa vya usafi binafsi
Masharti Muhimu ya Kuripoti Chuoni
- Hutapokelewa chuoni kama hutatekeleza masharti yote
- Ni lazima kufuata sheria na taratibu za chuo
- Uje na barua ya wito siku ya kuanza mafunzo
- Ada ya mitihani ya Taifa italipwa utakapojulishwa
- Nafasi itapotea ukishindwa kuripoti ndani ya wiki mbili
- Siku ya kuripoti uje na cheti halisi cha darasa la saba au kidato cha nne kwa uthibitisho
Sheria na Taratibu za Chuo (Kwa Muhtasari)
- Mahudhurio ya chini ya asilimia 85 hayaruhusu kufanya mtihani
- Kila mwanafunzi afike chuoni kabla ya saa 1:30 asubuhi
- Simu za mkononi haziruhusiwi darasani au karakana
- Sare ya chuo ni lazima kuvaliwa wakati wote wa mafunzo
- Mapambo, ulevi, wizi, ugomvi, dawa za kulevya, mapenzi chuoni na migomo ni marufuku
Kuzingatia mahitaji, ada na sheria hizi kutamwezesha mwanachuo kusoma katika mazingira bora na yenye nidhamu kwa mafanikio ya mafunzo ya ufundi stadi.




Leave a Reply
View Comments