Hizi hapa Fomu za Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2026 Kupitia TAMISEMI baada ya Matokeo ya Darasa la Saba 2025 NECTA yalipo tangazwa na jana walipo tangaza orodha ya waliochaguliwa kujiunga na form one na shule walizopangiwa wanafunzi wote wa bweni na kutwa Tanzania.
Kila mwaka baada ya NECTA kutangaza Matokeo ya Darasa la Saba 2025 (PSLE), wazazi na wanafunzi huanza hatua muhimu ya kuangalia mgawo wa shule (Selection) pamoja na kupakua fomu za kujiunga na Kidato cha Kwanza 2026 kupitia mfumo wa TAMISEMI. Hii ndiyo hatua inayowaruhusu wanafunzi kujiandaa rasmi kuanza safari yao ya elimu ya sekondari.
Hapa chini tumekuletea maelezo muhimu, hatua kwa hatua, ili kusaidia kuelewa vizuri mchakato wa TAMISEMI Selection and Allocation na jinsi ya kupata fomu za kujiunga (Joining Instructions).
Bofya hapa kuona na kudownload PDF za fomu za kujiunga na kila shule
Shule walizochaguliwa kidato cha kwanza nini maana yake?
Uchaguzi wa kidato cha kwanza 2026 ni zoezi la serikali kupitia Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) linalohusika kugawa wanafunzi wa Darasa la Saba waliomaliza elimu ya msingi kwenda:
- Shule za Sekondari za Serikali
- Shule za bweni
- Shule maalumu
- Shule za mchanganyiko (day & boarding)
Mgawo huu hutegemea mambo kama:
- Matokeo ya mwanafunzi (PSLE)
- Uchaguzi alizofanya awali (kama uliombwa)
- Upatikanaji wa nafasi katika shule husika
- Kipaumbele cha kitaifa — jinsia, mahitaji maalumu, umbali na miundombinu
Jinsi ya Kuangalia waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2026
Mara tu TAMISEMI wanapotangaza rasmi mgawo wa wanafunzi, unaweza kufuata hatua hizi rahisi:
Hatua za Kuangalia Selection
- Fungua tovuti ya TAMISEMI: https://selection.tamisemi.go.tz/allocations au https://tamisemi.go.tz
- Chagua menyu ya “Form One first Selection 2026”
- Chagua:
- Mikoa
- Wilaya
- Shule
- Tazama jina la mwanafunzi katika orodha ya waliochaguliwa.
Kupata Fomu za Kujiunga (Joining Instructions)
Baada ya kuthibitisha kuwa mwanafunzi amechaguliwa, hatua inayofuata ni kupakua na kuchapisha Fomu za Kujiunga. Hizi fomu zinajumuisha:
- Maelekezo ya shule
- Vifaa muhimu vya kuandaa (school requirements)
- Ada na mchango wa shule (ikiwa upo)
- Kanuni za shule
- Ratiba ya kuripoti
Jinsi ya Kupakua Joining Instructions
- Tembelea tovuti ya TAMISEMI: https://selection.tamisemi.go.tz/allocations/2025/first-selection/index.html
- Chagua mkoa kisha wilaya
- Chagua shule uliyosoma mfano PS0204054 – SINZA
- Bofya jina la shule uliyochaguliwa kupata Joining Instructions
- Bonyeza sehemu imeandikwa “Amechaguliwa kwenda”
- Bonyeza Download ili kupakua PDF.
Umuhimu wa Fomu hizi za Kujiunga
Fomu hizi ni muhimu kwa sababu:
- Ni lazima kuwasilishwa shuleni siku ya kuripoti
- Zinawaongoza wazazi/walezi kununua vifaa sahihi
- Hutoa maelekezo ya maadili na kanuni za shule
- Husaidia mwanafunzi kujiandaa kisaikolojia na kimatendo
Kuchelewa kuchukua au kupeleka fomu kunaweza kusababisha mwanafunzi kuchelewa kuanza masomo.
Hitimisho
Kupata fomu za kujiunga na Kidato cha Kwanza kupitia TAMISEMI ni hatua rahisi, ilimradi ujue wapi pa kuangalia na nini cha kufuata. Hakikisha unatembelea tovuti rasmi, unapakua fomu sahihi, na unamwandaa mwanafunzi kikamilifu kabla ya siku ya kuripoti.
TAMISEMI na NECTA wameweka mfumo rahisi unaowezesha wazazi na wanafunzi kupata taarifa kwa wakati, hivyo kuhakikisha mpito wa kuanza elimu ya sekondari unakwenda vizuri.
Soma zaidi:




Leave a Reply
View Comments