Nafasi za Kazi Jeshi la Magereza Tanzania 2025 PDF

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Jeshi la Magereza Tanzania limefungua rasmi nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) katika fani ya uhudumu wa jikoni kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali..

Tangazo hili limetolewa na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma tarehe 09 Disemba 2025, na mwisho wa kutuma maombi ni 23 Disemba 2025.

Jeshi la Magereza

Kuhusu, Jeshi la Magereza lilianzishwa rasmi mwezi Agosti 25,1931 baada ya mgawanyo wa majeshi ya Polisi na Magereza kutokea. Licha ya kuwa na majukumu ya kulinda usalama na mali za wageni, kabla ya mwaka 1931 Jeshi la Polisi lilifanya pia kazi za Magereza kama zilivyokuwa kwa tafsiri na madhumuni ya wakoloni. Jeshi la Magereza wakati lilipoanzishwa liliitwa Idara ya Jela ambapo shughuli zake zilibaki kuwa zile za kikoloni za utesaji wa wafungwa pamoja na kazi ngumu bila kujali kama ni ya manufaa kwao au kwa Taifa.

Sifa za Waombaji

  • Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne na cheti cha mafunzo ya uhudumu wa jikoni kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Fani na Ujuzi Unaohitajika

Jedwali lifuatalo linaonyesha fani zinazotakiwa kwa ngazi tofauti:

Ngazi ya ElimuFani Zinazohitajika
Kidaro cha NneMhudumu wa Jikoni Daraja la II

Jinsi ya Kutuma Maombi

Waombaji wote wanapaswa kuwasilisha maombi kupitia Mfumo wa Ajira Portal kupitia kiunganishi:

Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo huu hayatapokelewa.

Maelekezo Muhimu

  • Waombaji waliowahi kufukuzwa mafunzo ya awali ya uaskari hawaruhusiwi kuomba tena.
  • Mtu yeyote atakayewasilisha nyaraka za kughushi au taarifa za uongo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Mwisho wa Kutuma Maombi

23 Disemba 2025

Soma zaidi: