Orodha ya Fani zilizokubaliwa kufundishwa VETA 2026 vyuo pamoja na kozi zinazotolewa kwa chuo husika pamoja na ada ya kusoma au gharama.
Katika makala haya yameandaliwa kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi, wazazi, walezi na wadau wa mafunzo ya ufundi wanaotaka kujua vyuo ambavyo vimepitishwa rasmi na Serikali kutoa Mafunzo ya Uanagenzi kwa mwaka wa fedha 2025/26. Inalenga kutoa picha kamili ya vyuo vilivyokidhi vigezo vya ubora chini ya usimamizi wa VETA, pamoja na kuwasaidia wanaotaka kujiunga na mafunzo hayo kupanga uelekeo wao kwa ujuzi watakaoupata kupitia mfumo wa mafunzo kwa vitendo.
Fomu za maombi zinapatikana katika vyuo vyote vilivyopitishwa na Serikali kutoa mafunzo haya.
Vyuo vya VETA Arusha
1. Kituo cha Jemolojia (TGC)
Kozi zinazotolewa chuo cha TGC
- Ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito
- Usonara
- Utambuzi wa madini ya vito
2. Chuo cha Taifa cha Utalii – Kampasi ya Arusha
Kozi zinazotolewa Chuo cha Taifa cha Utalii
- Huduma ya vinywaji na chakula
- Mapokezi
- Usafi wa vyumba na udobi
- Utalii na Usafirishaji
- Kuongoza watalii
Vyuo vya VETA Dar es Salaam
1. Anna Collection Academy (AFA)
Kozi zinazotolewa chuo cha AFA
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
2. Don Bosco Oysterbay Vocational Training Centre
Kozi zinazotolewa chuo cha Don Bosco
- Upishi
- Uokaji
- Ufundi umeme wa majumbani
- Umeme wa jua
- Uchorongaji vipuri
- Ufundi magari
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
3. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kigamboni
Kozi zinazotolewa chuo cha Kigamboni
- Ufundi umeme wa majumbani
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Umeme wa magari
- Ufundi bomba
- Ufundi magari
Vyuo vya VETA Dodoma
1. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Chisalu
Kozi zinazotolewa chuo cha Chisalu
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Uashi
- Ufundi magari na mitambo
- Ufundi umeme wa majumbani
2. Institute of Heavy Equipment and Technology (IHET)
Kozi zinazotolewa chuo cha IHET
- Ufundi wa mitambo
- Uendeshaji wa mitambo
- Mashine za kunyanyua mizigo
- Umeme wa magari
3. Don Bosco Dodoma Technical Institute
Kozi zinazotolewa chuo cha Don Bosco Dodoma
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Ufundi bomba
- Uashi
- Useremala
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Uchorongaji vipuri
- Ufundi magari
- Ufundi umeme wa majumbani
- Kilimo cha mboga
Vuo vya VETA Geita
1. Chuo cha Ufundi Stadi Geita
Kozi zinazotolewa chuo cha Geita
- Ufundi umeme wa majumbani
- Umeme wa magari
- Ufundi magari
- Ufundi bomba
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
Vyuo vya VETA Iringa
1. Ifunda Tech School (VTC)
Kozi zinazotolewa chuo cha Ifunda
- Uchomeleaji
- Umeme wa magari
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ufundi bomba
- Ushonaji
2. Don Bosco Iringa Youth Training Centre
Kozi zinazotolewa chuo cha Don Bosco Iringa
- Ufundi umeme wa majumbani
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Ufundi magari
- Uchapishaji
- Ufundi bomba
- Kilimo
Vyuo vya VETA Kagera
1. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Rubondo
Kozi zinazotolewa chuo cha Rubondo
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Umeme wa magari
- Ufundi magari
2. VETA Karagwe
Kozi zinazotolewa chuo cha VETA Karagwe
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Ufundi magari
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ufundi vifaa vya kielectroniki
- Umeme wa magari
Vyuo vya VETA Katavi
1. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Msaginya
Kozi zinazotolewa chuo cha Msaginya
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ushonaji
- Upishi
- Kilimo
- Ufundi bomba
Vyuo vya VETA Kigoma
1. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kasulu
Kozi zinazotolewa chuo cha Kasulu
- Ufundi umeme wa majumbani
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Umeme wa magari
- Ufundi bomba
- Ufundi magari
- Ususi na urembo
2. VETA Kigoma
Kozi zinazotolewa chuo cha VETA Kigoma
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Ufundi bomba
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Ufundi magari na mitambo
- Ufundi umeme wa majumbani na viwandani
Vyuo vya VETA Kilimanjaro
1. Marangu School of Tourism
Kozi zinazotolewa chuo cha Marangu
- Kuongoza watalii
- Upishi
- Huduma ya chakula na vinywaji
- Huduma ya kupokea wageni
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ususi na urembo
2. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mamtukuna
Kozi zinazotolewa chuo cha Mamtukuna
- Ufundi magari
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Kilimo
Vyuo vya VETA Lindi
1. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko
Kozi zinazotolewa chuo cha Kilwa Masoko
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Ufundi magari na mitambo
- Ufundi umeme wa majumbani
- Huduma za Hoteli na Utalii
Vyuo vya VETA Manyara
1. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Tango
Kozi zinazotolewa chuo cha Tango
- Ufundi umeme wa majumbani na viwandani
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Ufundi magari na mitambo
- Kilimo
Vyuo vya VETA Mara
1. Chuo cha Mafunzo Musoma Utalii
Kozi zinazotolewa Chuo cha Mafunzo Musoma Utalii
- Kuongoza watalii
- Upishi
2. St. Anthony Vocational Training Centre
Kozi zinazotolewa St. Anthony Vocational Training Centre
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ufundi magari
- Ufundi bomba
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Umeme wa magari
Vyuo vya VETA Mbeya
1. Mbeya University of Science and Technology (MUST)
Kozi zinazotolewa Chuo cha MUST
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Ufundi magari na mitambo
- Umeme wa magari
- Umeme wa majumbani na viwandani
- Ufundi bomba
- Ufundi vifaa vya aluminium
- Upakaji rangi na maandishi
2. Kyela Polytechnic College
Kozi zinazotolewa chuo cha Kyela
- Ufundi magari
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ususi na urembo
3. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Nzovwe
Kozi zinazotolewa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Nzovwe
- Useremala
- Kilimo
- Ufundi umeme wa majumbani na viwandani
Vyuo vya VETA Morogoro
1. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa
Kozi zinazotolewa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Upishi
- Kilimo
- Mifugo
- Ufundi magari
2. Mzinga Vocational Training Centre
Kozi zinazotolewa chuo cha Mzinga
- Utengenezaji wa vipuri na mitambo
- Ufundi wa magari na mitambo
- Umeme wa magari
3. Lakewood Vocational Training College
Kozi zinazotolewa chuo cha Lakewood
- Kuongoza watalii
- Ufundi umeme wa majumbani
Vyuo vya VETA Mtwara
1. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mtawanya
Kozi zinazotolewa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mtawanya
- Ufundi umeme wa majumbani na viwandani
- Ufundi bomba
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Ufundi magari
- Umeme wa magari
2. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Newala
Kozi zinazotolewa na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Newala
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ufundi magari
- Ushonaji
- Uashi
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Utengenezaji wa samani
- Ufundi vifaa vya aluminium na PVC
Vyuo vya VETA Mwanza
1. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sengerema
Kozi zinazotolewa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sengerema
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ufundi bomba
- Ufundi magari
- Umeme wa magari
- Ushonaji nguo
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
2. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malya
Kozi zinazotolewa chuo cha Malya
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ufundi bomba
- Kilimo na ufugaji
- Uashi
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
3. Stadi Pine College
Kozi zinazotolea chuo cha Stadi Pine
- Umeme wa majumbani na viwandani
- Ushonaji nguo
- Ufundi bomba
- Umeme wa magari
Vyuo vya VETA Njombe
1. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Njombe
Kozi zinazotolewa Chuo cha Njombe
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ufundi magari
- Umeme wa magari
Vyuo vya VETA Pwani
1. Vikindu Catholic Polytechnic College
Kozi zinazotolewa Chuo cha Vikindu
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ufundi bomba
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Ufundi umeme wa magari
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Upakaji rangi na maandishi
Vyuo vya VETA Ruvuma
1. Peramiho VTC
Kozi zinazotolewa Chuo cha Peramiho VTC
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Ufundi bomba
- Useremala
- Ufundi magari
- Ufundi umeme wa majumbani
2. St. Joseph VTC
Kozi zinazotolewa chuo cha St. Joseph VTC
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ufundi bomba
- Ufundi magari
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Umeme wa magari
Vyuo vya VETA Shinyanga
1. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mwanva
Kozi zinazotolewa chuo cha Shinyanga
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ufundi bomba
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Ufundi magari
2. Chuo cha Hill Forest – Shinyanga
Kozi zinazotolewa Chuo cha Hill Forest
- Mapokezi
Vyuo vya VETA Singida
1. Chuo cha Ufundi na Marekebisho Sabasaba
Kozi zinazotolewa Chuo cha Ufundi na Marekebisho Sabasaba
- Ususi na urembo
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Ufundi wa simu na vifaa vya kielectroniki
- Ufundi umeme wa majumbani
- Upishi
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
2. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Singida
Kozi zinazotolewa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Singida
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ufugaji wa wanyama na nyuki
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Ufundi magari
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
Vyuo vya VETA Songwe
1. Chuo cha Ufundi Stadi Songwe
Kozi zinazotolewa Chuo cha Ufundi Stadi Songwe
- Ususi na urembo
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Ufundi umeme wa majumbani
- Kuongoza watalii
Vyuo vya VETA Rukwa
1. Chuo cha Kilimo Laela
Kozi zinazotolewa Chuo cha Kilimo Laela
- Kilimo
- Mifugo
Vyuo vya VETA Tabora
1. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sikonge
Kozi zinazotolewa chuo cha Sikonge
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
- Ufundi bomba
- Ufundi umeme wa majumbani
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
2. VETA Urambo
Kozi zinazotolewa chuo cha VETA Urambo
- Ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo
- Ufundi umeme wa majumbani
Vyuo vya VETA Tanga
1. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Handeni
Kozi zinazotolewa Chuo cha Handeni
- Ufundi umeme wa majumbani
- Uashi
- Ufundi magari
- Ushonaji
- Ufundi bomba
- Uchomeleaji na uungaji vyuma
Soma zaidi:
Makala hii imeandaliwa kwa ajili ya:
- Wanafunzi wanaotaka kujiunga na Mafunzo ya Uanagenzi (Apprenticeship Training) nchini Tanzania.
- Wazazi na walezi wanaotafuta taarifa sahihi kuhusu vyuo vinavyotambulika na serikali.
- Waajiri na wadau wa sekta ya ujuzi wanaohitaji kujua vyuo vinavyokidhi vigezo vya kutoa mafunzo kwa vitendo.
Makala inaeleza kwa ufupi kuhusu VETA—mamlaka inayoongoza mafunzo ya ufundi stadi nchini—na pia inatoa orodha kamili ya vyuo vilivyopendekezwa na serikali kwa awamu ya nane, mwaka wa fedha 2025/26.
VETA ni Nini na Inasimamia Nini?
VETA (Vocational Education and Training Authority) ni mamlaka ya serikali yenye jukumu la:
- Kusimamia na kuratibu mafunzo ya ufundi stadi nchini Tanzania.
- Kupitisha na kuratibu vyuo vinavyotoa kozi za ufundi na uanagenzi.
- Kuhakikisha mafunzo yanaendana na viwango vya soko la ajira na mahitaji ya kitaifa.
- Kutoa leseni, usimamizi wa mitaala, na kuhakikisha ubora wa mafunzo ya ufundi.




Leave a Reply
View Comments