Hizi hapa Shule Walizopangiwa kidato cha kwanza Darasa la Saba 2026 NECTA Baada ya kutangazwa kwa Matokeo ya Darasa la Saba 2025 pamoja na fomu za kujiunga na Baraza la Mitihani la Taifa, hatua inayofuata ni upangaji wa wanafunzi katika shule za sekondari waliochaguliwa kidato cha kwanza ama form one selectio 2026. Mchakato huu hufanywa kitaifa na kuongozwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na TAMISEMI pamoja na Ofisi za Elimu za Mikoa na Wilaya husika.
Maana ya Upangaji wa Shule za kidato cha kwanza
- Ni hatua ya kugawa wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi katika shule za sekondari kulingana na ufaulu wao.
- Hufanywa kwa kuzingatia nafasi zilizopo katika shule mbalimbali za serikali na binafsi.
- Pia huangalia jinsia, eneo la mwanafunzi, na shule aliyoomba awali (ikiwa alichagua).
Uchaguzi wa wanafunzi kidato cha kwanza 2026 form one angalia hapa
Jinsi ya Kuangalia Shule Walizopangiwa 2025/26
Ili kujua shule uliyopangiwa baada ya matokeo ya matokeo ya darasa la saba 2025:
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA au TAMISEMI: www.necta.go.tz au: https://selection.tamisemi.go.tz/allocations
- Tafuta kipengele chenye maandishi “Selection Results 2025” au “Shule Walizopangiwa Wanafunzi wa Darasa la Saba 2025”.
- Bonyeza kiungo hicho na uchague Mkoa wako.
- Baada ya hapo, chagua Wilaya yako.
- Unaweza pakua ama kudownload fomu za kujiunga na kidato cha kwanza hapo hapo
- Orodha ya wanafunzi waliopangiwa shule itaonekana, ikionyesha jina la mwanafunzi, namba ya mtihani, na shule aliyopangiwa.
Mambo ya Kuzingatia Baada ya kuchaguliwa Shule za kutwa na Bweni
- Hakikisha unathibitisha jina lako na shule uliyopewa ili kuepuka makosa ya taarifa.
- Wazazi au walezi wanapaswa kuanza maandalizi ya ada, sare, na vifaa vya shule mapema.
- Wanafunzi wanaopangiwa mbali na makazi yao wanashauriwa kuripoti kwa wakati ili kuepuka kuchelewa masomo.
Kumbuka: Ikiwa huwezi kupata orodha kamili ya waliochaguliwa kidato cha kwanza 2026 mtandaoni, unaweza kuyaona moja kwa moja shuleni kwako.
Umuhimu wa Mchakato wa Upangaji
- Unatoa nafasi kwa wanafunzi wote nchini kuendelea na elimu ya sekondari kwa usawa.
- Unasaidia serikali kupanga rasilimali na miundombinu ya elimu kulingana na idadi ya wanafunzi wapya.
- Pia husaidia wazazi na walimu kufuatilia maendeleo ya elimu kwa ngazi ya taifa.
Hitimisho
Shule walizochaguliwa wanafunzi wa kidato cha kwanza au Darasa la Saba 2025 2026 ni hatua muhimu katika safari ya elimu nchini Tanzania. Wazazi, walimu, na wanafunzi wanapaswa kufuatilia taarifa hizi kwa umakini na kuhakikisha maandalizi yote yanakamilika kabla ya shule kufunguliwa.
Soma zaidi:




Leave a Reply
View Comments