Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mafunzo ya Ufundi Sura ya 82. Kazi yake kubwa ni kutoa, kuratibu na kufadhili mafunzo ya ufundi stadi nchini.
Dira (Vision)
“Tanzania yenye mafundi stadi wa kutosha na wenye uwezo.”
Dhamira (Mission)
“Kuhakikisha Tanzania inapata watu wenye ujuzi wa ufundi kupitia utoaji na uhamasishaji wa Mafunzo ya Ufundi Stadi ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi.”
Maadili Yetu ya Msingi
1. Watu Kwanza
Tunajitahidi kutimiza matarajio ya wananchi kwa unyenyekevu, staha na kuwahudumia kwa haraka.
2. Ujuzi na Ubunifu
Tumejikita kuongeza ujuzi wa vitendo ili kukabiliana na teknolojia mpya na mahitaji ya soko la ajira.
3. Kufanya Kazi kwa Pamoja na Uadilifu
Tunaamini katika ushirikiano, kufanya kazi kwa uaminifu wa hali ya juu ili kufikia malengo ya pamoja.
4. Uhusika (Relevancy)
Tunajitahidi kutoa mafunzo na huduma zinazolingana na mahitaji ya soko la ajira na watu kwa ujumla.
Majukumu ya VETA
i. Kutoa Mafunzo ya Ufundi Stadi
VETA inaendesha mafunzo kupitia vituo vyake vilivyopo kote nchini. Walimu wa ufundi huzalishwa kupitia Chuo Maalum cha Ualimu wa Ufundi cha Morogoro (MVTTC).
ii. Kusaidia Upatikanaji wa Fedha za Mafunzo ya Ufundi
VETA husaidia upatikanaji wa fedha kupitia mfuko wa Skills Development Levy (SDL)—michango inayotolewa na waajiri kutoka kwenye mishahara ya wafanyakazi wao. Fedha zingine zinatoka kwenye miradi ya serikali, wafadhili, ada za mafunzo na shughuli za kujipatia kipato.
iii. Kukuza na Kuhamasisha Mafunzo ya Ufundi
VETA ina jukumu la kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa mafunzo ya ufundi. Wanatoa taarifa kwa wadau mbalimbali kama serikali, waajiri, wazazi, wanafunzi, wahitimu, wafanyakazi, vyama vya wafanyakazi, NGOs na vyombo vya habari.
Uhamasishaji hufanyika kupitia matangazo, makongamano, maonyesho, VET Week, mitandao ya kijamii, tovuti, mabrosha, ripoti na machapisho mbalimbali.
Utoaji wa Mafunzo
Mafunzo ya VETA yanatolewa katika sekta 13 za kazi, ambazo ni:
- Ufundi Mitambo
- Umeme
- Ujenzi
- Magari
- Huduma za Biashara
- Ushonaji na Textile
- Usafirishaji
- Madini
- Uchapaji
- Urembo na Uanamitindo
- Kilimo na Uchakataji wa Mazao
- Utalii, Hoteli na Usafiri
- Sanaa na Michezo
