Kozi za VETA Bahi 2026: Muda na Ada

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa waliochaguliwa kidato cha tano 2026, Matokeo ya kidato cha sita 2026 kujiunga na vyuo, nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Fahamu orodha ya kozi za VETA Bahi 2026, muda wa mafunzo na ada zake. Chuo cha Ufundi Stadi Bahi kinatoa mafunzo ya ufundi stadi katika fani mbalimbali zinazowawezesha wanafunzi kupata ujuzi wa vitendo kwa ajili ya kujiajiri au kuajiriwa.

Bonyeza hapa kutuma maombi ya VETA Bahi 2026

Kozi zinazotolewa chuoni hapo zinahusisha matumizi ya kompyuta, ufundi magari, ubunifu wa mavazi na ushonaji, ufundi umeme, ujenzi, uungaji vyuma, udereva pamoja na ujasiriamali, ufugaji na kilimo.

Orodha ya Kozi za VETA Bahi 2026

Hapa chini ni orodha ya kozi zinazotolewa katika Chuo cha Ufundi Stadi Bahi, muda wa mafunzo na ada zake.

Na.Jina la KoziMuda wa MafunzoAda (TSh)
1Kompyuta (Basic Computer Applications)Wiki 8250,000
2Ufundi Magari (Motor Vehicle Mechanics)Miezi 3300,000
3Ubunifu wa Mavazi, Ushonaji na Teknolojia ya NguoMiezi 3300,000
4Ufundi Umeme (Electrical Installation)Miezi 3300,000
5Ujenzi (Masonry and Bricklaying)Miezi 3300,000
6Uundaji na Uungaji Vyuma (Welding and Metal Fabrication)Miezi 3300,000
7Udereva wa Pikipiki na Bajaji (Motorcycle and Tricycle Riding)Wiki 140,000
8Udereva wa Awali (Basic Driving)Wiki 5245,000
9Ujasiriamali, Ufugaji na Kilimo (Entrepreneurship Skills)Wiki 4200,000

Jinsi ya Kutuma Maombi ya Kujiunga na VETA Bahi

Waombaji wanaotaka kujiunga na Chuo cha Ufundi Stadi Bahi wanaweza kutuma maombi kupitia mfumo rasmi wa VETA kwa kutumia kiungo kifuatacho.

Unashauriwa kufuata maelekezo yaliyopo kwenye mfumo na kuchagua kozi unayotaka kusomea.

Mawasiliano ya Chuo cha VETA Bahi

Kwa maelezo zaidi kuhusu kozi zinazotolewa, ada, udahili na masharti ya kujiunga, unaweza kuwasiliana na chuo kupitia mawasiliano yafuatayo:

  • Jina la Chuo: Chuo cha Ufundi Stadi Bahi
  • Anuani: Bahi, Tanzania
  • Simu: 0675 231 784 / 0769 895 643
  • Barua pepe: bahidvtc@veta.go.tz

Hitimisho

VETA Bahi inatoa fursa ya kujifunza fani mbalimbali za ufundi stadi kwa muda tofauti kulingana na kozi husika. Waombaji wanaweza kuchagua kozi inayolingana na malengo yao, muda wanaoweza kutumia katika mafunzo na uwezo wa kulipa ada. Kwa taarifa zaidi kuhusu udahili, wasiliana moja kwa moja na chuo kupitia namba za simu au barua pepe zilizotolewa hapo juu.

Soma zaidi: Kozi za VETA Geita 2026: Muda na Ada