Walioitwa kwenye Usaili TIRA 2026

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa waliochaguliwa kidato cha tano 2026, Matokeo ya kidato cha sita 2026 kujiunga na vyuo, nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ilitangaza nafasi za kazi za uhamisho tarehe 16 Desemba 2025 na kuwaalika watumishi wa umma wenye sifa na wanaotamani kufanya kazi TIRA kuwasilisha maombi yao kuanzia tarehe 16 Desemba 2025 hadi tarehe 31 Desemba 2025 saa 11:00 jioni.

Waombaji walioteuliwa kuingia kwenye orodha fupi (shortlisted) wanataarifiwa kuhudhuria usaili wa maandishi na wa mahojiano (mdomo) katika tarehe na muda ulioainishwa hapa chini.

Aidha, waombaji wote walioteuliwa wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:

  1. Kufika na vyeti vyao halisi, ikiwemo cheti cha kuzaliwa, vyeti vya elimu kuanzia elimu ya sekondari hadi kiwango cha juu cha elimu walichofikia, pamoja na kitambulisho cha Taifa, kitambulisho cha mpiga kura, pasipoti au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji.
  2. Nyaraka kama Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na Results Slips hazitakubaliwa.
  3. Waombaji watagharamia wenyewe gharama zote za malazi, chakula cha mchana na usafiri.
  4. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanatakiwa kuhakikisha vyeti vyao vya elimu vimethibitishwa na mamlaka husika, ambazo ni Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), au Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
  5. Usaili wa maandishi utafanyika tarehe 19 Juni 2026, na waombaji watakaofaulu watafanya usaili wa mahojiano (mdomo) tarehe 20 Juni 2026.
  6. Waombaji ambao majina yao hayajaonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo vilivyohitajika.

Pakua PDF hapa

Soma zaidi: Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita 2026