Hili hapa tangazo la Nafasi 5,476 za Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano inatekeleza Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi ambayo inalenga kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupata ujuzi wa stadi za kazi stahiki ili kuweza kushindana katika soko la ajira. Katika kutekeleza programu hii, Ofisi imeingia makubaliano na vyuo 46 vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi yaliyoidhinishwa na Serikali.
Mafunzo haya yanatolewa katika fani mbalimbali zikiwemo:
- Urembo na Ususi
- Ushonaji nguo na ubunifu wa mitindo
- Ufundi bomba
- Uashi
- Fundi magari
- Ujenzi
- Useremala
- Uungaji vyuma
- Uchomeleaji
- Upakaji rangi
- Maandishi ya alama
- Upishi
- Utengenezaji wa vipuri vya mitambo
- Umeme wa majumbani na viwandani
- Umeme wa magari
- Umeme wa jua (solar)
- Huduma za hoteli na utalii
- Ukataji madini
- Ufundi vyuma na fani nyingine zinazohusiana
Serikali itagharamia ada za mafunzo kwa asilimia 100. Mwanafunzi/Mzazi/Mlezi atawajibika kugharamia gharama nyingine kama nauli ya kwenda na kurudi chuo.
Mafunzo yatadumu hadi tarehe 26 Januari 2026.
Waombaji wanatakiwa kuchukua fomu katika Vituo vya Ufundi Stadi (VETA) vya Mikoa na Wilaya vilivyopitishwa na Serikali ambavyo vimeorodheshwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu: www.kazi.go.tz.
Vituo Vilivyopitishwa
Vyuo vyote 46 vilivyokubaliwa na Serikali kutoa mafunzo hivi vimepewa idhini rasmi kuendesha mafunzo haya katika fani husika.
Masharti ya Kujiunga na Mafunzo
- Awe Mtanzania.
- Awe na umri kati ya miaka 15 hadi 35.
- Awe mwenye afya njema.
- Awe na elimu ya msingi au zaidi kwa fani za ubunifu wa mitindo, ushonaji nguo, ufundi bomba, ujenzi, useremala, uchomeleaji, uungaji vyuma, upakaji rangi, maandishi ya alama, upishi na kadhalika.
- Kwa fani nyingine zinazohitaji kiwango cha elimu ya sekondari, mwombaji awe amemaliza kidato cha nne au zaidi.
- Vijana wenye ulemavu wamehimizwa sana kuomba na watapewa kipaumbele.
Jinsi ya Kuomba
Maombi yatawasilishwa kuanzia tarehe 05 hadi 19 Desemba 2025 kwa kuambatanisha:
- Barua ya maombi ya mafunzo;
- Nakala ya Cheti cha kuzaliwa;
- Nakala ya Cheti cha elimu uliyohitimu;
- Kitambulisho cha uraia / kadi ya mpiga kura (kwa wenye miaka 18+);
- Barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji anakoishi mwombaji;
- Picha nne za pasipoti (ziandikwe majina matatu ya mwombaji nyuma).
Maombi yapelekwe katika Chuo kilichopo katika mkoa unakoishi ambacho kimeteuliwa na Serikali kutoa mafunzo haya.
Uteuzi wa Waombaji
Waombaji wote watakaokidhi vigezo vilivyotajwa ndiyo watakaopangiwa nafasi.
Leave a Reply
View Comments