Hii hapa fomu na Jinsi ya Kujiunga na Chuo cha VETA Butiama 2026: Ada, Mahitaji na Sheria Muhimu
Kujiunga na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA Butiama) ni fursa muhimu kwa vijana wanaotaka kupata ujuzi wa vitendo unaohitajika kwenye soko la ajira. Makala hii inaeleza muda wa mafunzo, tarehe ya kuripoti, ada, mahitaji ya kujiunga na sheria za chuo kwa mwaka 2026 kwa ufupi na kwa kueleweka.
Bonyeza hapa kupakua fomu ya veta chuo cha Butiama PDF
Soma zaidi:
Mahitaji Muhimu kwa Mwanafunzi Ukiwa Chuoni (Muhtasari)
Sare ya Chuo
Unatakiwa kununua na kuwa na sare zifuatazo:
- Mashati mawili meupe ya mikono mifupi (kitambaa cha tetroni)
- Suruali mbili za rangi ya bluu iliyokoza (zinapatikana chuoni)
- Jozi moja ya viatu vyeusi vya ngozi vyenye visigino vifupi (kwa masomo ya darasani)
- Ovaroli moja ya rangi ya bluu iliyokoza (inapatikana chuoni)
- Soksi ndefu jozi mbili za rangi nyeupe
- Sweta moja la rangi ya bluu iliyokoza (linapatikana chuoni)
Vifaa Vingine vya Masomo
- Madaftari makubwa saba (7) aina ya 3Q
- Mathematical set
- Kalamu za wino na penseli (2B na HB) za kutosha
- Rimu moja ya karatasi A4 (Double A au Mapacha) – itakabidhiwa ofisini
Malipo ya Ada na Michango ya Chuo
Malipo yote yatafanyika kupitia Control Number itakayotolewa chuoni
(isipokuwa Bima ya Afya – NHIF)
Jedwali la Malipo
| Na | Aina ya Malipo | Muhula I (TSh) | Muhula II (TSh) |
|---|---|---|---|
| i | Ada ya Mafunzo (Kutwa) | 30,000 | 30,000 |
| ii | Ada ya Mafunzo (Bweni) | 60,000 | 60,000 |
| iii | Fedha ya Uchakavu | 10,000 | – |
| iv | Vifaa vya Michezo | 10,000 | – |
| v | Vifaa vya Usafi | 10,000 | – |
| vi | Bima ya Afya (NHIF) | 50,400 | – |
| vii | Suruali mbili (dark blue) | 40,000 | – |
| viii | T-Shirt ya VETA | 16,000 | – |
| ix | Ovaroli (dark blue) | 30,000 | – |
| x | Kitambulisho (ID) | 5,000 | – |
| xi | Nembo ya VETA | 5,000 | – |
| xii | Sweta (V-shape) | 16,000 | – |
| Jumla Kutwa | 222,400 | 30,000 | |
| Jumla Bweni | 252,400 | 60,000 |
Mahitaji ya Ziada kwa Wanafunzi wa Bweni
- Vyombo vya chakula (sahani, bakuli, kikombe, kijiko)
- Shuka mbili, blanketi na chandarua
- Ndoo, beseni na vifaa vya usafi binafsi
Sheria Muhimu za Chuo (Kwa Ufupi)
- Mwanafunzi afike chuoni kabla ya saa 1:30 asubuhi
- Mahudhurio yasipungue 85% ili kuruhusiwa kufanya mitihani
- Sare ya chuo ni ya lazima wakati wote chuoni
- Mapambo, ulevi, wizi, ugomvi, mapenzi chuoni na migomo ni makosa makubwa
- Simu za mkononi haziruhusiwi wakati wa vipindi
Mwanafunzi hatapokelewa chuoni endapo hatatekeleza masharti yote yaliyotajwa hapo juu.




Leave a Reply
View Comments