Ajira Mpya Halmashauri ya Wilaya ya Urambo 2026

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa waliochaguliwa kidato cha tano 2026, Matokeo ya kidato cha sita 2026 kujiunga na vyuo, nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Halmashauri ya Wilaya ya Urambo imetangaza nafasi 4 za ajira kwa Dereva Daraja la II na Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II. Tuma maombi kupitia Ajira Portal kabla ya 10 Septemba 2026.

Bonyeza hapa kupakua PDF ya tangazo la ajira Halmashauri Urambo

Tangazo la Ajira Halmashauri ya Wilaya ya Urambo 2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi 4 za ajira baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Nafasi hizi zinahusisha kada za Dereva Daraja la II na Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II.

Muhtasari wa Nafasi za Kazi

KadaNafasiMshahara
Dereva Daraja la II3TGS B
Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II1TGS C

1. Dereva Daraja la II (Nafasi 3)

Majukumu ya kazi

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari.
  • Kuwasafirisha watumishi kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogo ya gari.
  • Kutunza daftari la safari (Log Book).
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka.
  • Kufanya usafi wa gari.
  • Kutekeleza majukumu mengine atakayopewa na msimamizi.

Sifa za mwombaji

Mwombaji anatakiwa kuwa na:

  • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
  • Leseni ya udereva Daraja C au E.
  • Uzoefu wa kuendesha gari usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
  • Cheti cha Basic Driving Course kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
  • Vyeti vya mafunzo vilivyomwezesha kupata madaraja ya leseni husika.

Ngazi ya mshahara: TGS B

2. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II (Nafasi 1)

Majukumu ya kazi

  • Kuchapa barua na nyaraka za kawaida na siri.
  • Kupokea na kuelekeza wageni.
  • Kutunza kumbukumbu za miadi, vikao na safari.
  • Kutafuta na kusambaza majalada.
  • Kuandaa dondoo za vikao.
  • Kuandaa mahitaji ya vifaa vya ofisi.

Sifa za mwombaji

Mwombaji anatakiwa kuwa na:

  • Elimu ya Kidato cha Nne au Sita.
  • Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6.
  • Uwezo wa Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza kwa maneno 100 kwa dakika.
  • Ujuzi wa programu za kompyuta: Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher.

Ngazi ya mshahara: TGS C

Masharti ya Jumla

Waombaji wote wanapaswa kuzingatia masharti yafuatayo:

  • Awe raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18–45.
  • Kuambatisha CV, namba ya simu, barua pepe na wadhamini watatu.
  • Kuambatisha vyeti halisi vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa.
  • Testimonials, Provisional Results na Result Slips hazitakubaliwa.
  • Waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vimeidhinishwa na TCU, NECTA au NACTVET.
  • Waombaji wa kada ya Dereva waambatishe vyeti vya mafunzo ya udereva.
  • Majina yanayotofautiana kwenye vyeti yaambatane na Deed Poll iliyosajiliwa.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Maombi yote yatumwe kwa njia ya kielektroniki kupitia Ajira Portal.

Anuani ya barua ya maombi:

Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo
S.L.P. 170
Urambo, Tabora

Muhimu: Maombi yanayotumwa nje ya mfumo rasmi wa Ajira Portal hayatashughulikiwa.

Tarehe ya Mwisho ya Kutuma Maombi

Mwisho wa maombi 10 Septemba 2026

Waombaji wanashauriwa kutuma maombi yao mapema kabla ya tarehe ya mwisho ili kuepuka changamoto za mfumo.

Soma zaidi: Matokeo ya Usaili Ajira Portal Aug 28-29