Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) kimetangaza ratiba ya kufunguliwa kwa mwaka wa masomo 2026/2027. Angalia tarehe za kuripoti, usajili na mafunzo elekezi.
Bonyeza hapa kuangalia ratiba kamili ya kufunguliwa Chuo cha TICD
Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) kimetangaza ratiba rasmi ya kufunguliwa kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na wanaoendelea na masomo katika Kampasi Kuu ya Tengeru, Buhare na kampasi zote za TICD kwa mwaka wa masomo 2026/2027.
Ratiba hii inaonesha tarehe za kuripoti chuoni, usajili kwa njia ya mtandao pamoja na mafunzo elekezi kwa ngazi mbalimbali za masomo.
Ratiba Rasmi ya Kufunguliwa TICD 2026/2027
| Tarehe | Wahusika | Kampasi/Tukio |
|---|---|---|
| 12 Oktoba 2026 | Cheti cha Awali (NTA Level 4) | Kampasi zote za TICD |
| 19 Oktoba 2026 | Shahada za Awali (NTA Level 7) | Kampasi Kuu Tengeru na Buhare |
| 19–27 Oktoba 2026 | Shahada za Uzamili (Masters) | Usajili kwa njia ya mtandao |
| 19 Oktoba 2026 | NTA Level 5, 6, 7(ii) na 8 | Kampasi zote za TICD |
| 26–30 Oktoba 2026 | Cheti cha Awali (NTA Level 4) | Mafunzo Elekezi – Kampasi zote |
| 26–30 Oktoba 2026 | Shahada za Awali (NTA Level 7) | Mafunzo Elekezi – Tengeru na Buhare |
| 28–29 Oktoba 2026 | Shahada za Uzamili (Masters) | Mafunzo Elekezi – Kampasi Kuu Tengeru |
Wanaotakiwa Kuripoti
Ratiba hii inawahusu makundi yafuatayo:
- Wanafunzi wapya wa Cheti cha Awali (NTA Level 4)
- Wanafunzi wa NTA Level 5, 6, 7(ii) na 8
- Wanafunzi wa Shahada za Awali
- Wanafunzi wa Shahada za Uzamili (Masters)
Kila mwanafunzi anatakiwa kuripoti katika tarehe iliyopangwa kwa ngazi yake ya masomo na kukamilisha usajili kabla ya kuanza masomo.
Mafunzo Elekezi
Mafunzo elekezi yatafanyika kuanzia 26 hadi 30 Oktoba 2026 kwa wanafunzi wa Cheti na Shahada za Awali, huku wanafunzi wa Shahada za Uzamili wakifanya mafunzo yao tarehe 28–29 Oktoba 2026 katika Kampasi Kuu ya Tengeru.
Hitimisho
Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) kwa mwaka wa masomo 2026/2027 wanashauriwa kuzingatia ratiba ya kuripoti, kukamilisha usajili kwa wakati na kuhudhuria mafunzo elekezi kama yalivyopangwa na chuo.
Soma zaidi: Walioitwa Kazini Sekretarieti ya Ajira Sept 16-21




Leave a Reply
View Comments