Nafasi za Kujitolea Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ilianzishwa rasmi chini ya Tangazo la Serikali Na. 453 la mwaka 2015 lililochapishwa gazetini na Serikali tarehe 16 Oktoba 2015 kama hospitali ya rufaa ya ngazi ya juu (tertiary referral hospital), ikiwa na lengo la kukidhi hitaji la huduma za afya za kibingwa na za juu nchini Tanzania. Huduma hizi hutolewa kupitia upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa kitabibu vya teknolojia ya hali ya juu, watumishi wenye ujuzi pamoja na matibabu ya kiwango cha juu.
Hospitali ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 400 waliolazwa na pia hutoa huduma kwa wagonjwa wa nje kutoka ndani na nje ya nchi. Kwa sasa, hospitali inatoa huduma mbalimbali za afya ikiwa ni pamoja na tiba za dharura, Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), huduma za picha za uchunguzi kama vile MRI (Magnetic Resonance Imaging), CT Scan (Computerized Tomography Scan), Mammography, X-ray, Ultrasound, angiography, Cath-lab, huduma za maabara, huduma za upasuaji pamoja na huduma za tiba ya mionzi (radiotherapy).
Kwa madhumuni ya kuboresha ufanisi wa utendaji kazi, hospitali inatafuta Watanzania wenye nguvu, ari na ubunifu kujaza nafasi zifuatazo za kujitolea (Volunteer): –
Nafasi zilizotangazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa
1. Muuguzi Daraja la II – Nafasi 14
2. Wasaidizi wa Muuguzi Daraja la II – Nafasi 10
Soma zaidi: Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)




Leave a Reply
View Comments