Kozi za VETA Tanga 2026: Muda na Ada

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa waliochaguliwa kidato cha tano 2026, Matokeo ya kidato cha sita 2026 kujiunga na vyuo, nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Fahamu orodha ya kozi za VETA Tanga 2026, muda wa mafunzo na ada zake kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi. Chuo cha Ufundi Stadi Tanga (Tanga RVTSC) kinatoa kozi mbalimbali zinazohusiana na udereva, ufundi wa magari, umeme, kompyuta, ujenzi, upishi, utalii na fani nyingine.

Bonyeza hapa kutuma maombi Chuo cha VETA Tanga 2026

Wanafunzi wanaweza kuchagua kozi kulingana na malengo yao ya kujifunza ujuzi wa kazi na kujiajiri au kuajiriwa.

Orodha ya Kozi za VETA Tanga 2026 na Ada Zake

Chuo cha VETA Tanga kinatoa kozi zenye muda tofauti wa mafunzo na ada kulingana na fani. Jedwali lifuatalo linaonyesha orodha ya kozi, muda wa mafunzo na ada zilizotolewa.

Na.Jina la KoziMuda wa MafunzoAda (TSh)
1Udereva wa Awali (Basic Driving of Motor Vehicle)Wiki 5232,000
2Udereva wa Magari ya Abiria (PSV)Wiki 2235,000
3Ufundi wa Magari (Motor Vehicle Mechanics)Miezi 6386,000
4Ufundi Umeme (Electrical Installation)Miezi 6386,000
5Useremala (Carpentry and Joinery)Miezi 6316,000
6Ufundi wa Umeme wa Magari (Auto-Electricity)Miezi 6386,000
7Upakaji Rangi na Uchoraji (Painting and Sign Writing)Miezi 6316,000
8Uhazili (Computer and Secretarial)Miezi 6351,000
9Ushonaji (Designing, Sewing and Cloth Technology)Miezi 3286,000
10Matumizi ya Kompyuta (Computer Application – Programu Saba)Miezi 3305,000
11Uchomeleaji Vyuma (Welding and Metal Fabrication)Miezi 6336,000
12Ufundi Bomba (Plumbing and Drainage)Miezi 6336,000
13Ufundi Uashi (Masonry and Brick Laying)Miezi 6316,000
14Utunzaji wa Vyumba/Nyumba (Housekeeping)Miezi 3306,000
15Mapokezi ya Wageni na Kompyuta (Front Office Operation and CA)Miezi 3378,000
16Mapishi (Food Production)Miezi 3296,000
17Huduma za Vyakula na Vinywaji (Food and Beverage Services)Miezi 3316,000
18Uokaji na Ukaangaji (Basic Bakery and Pastry Production)Miezi 3406,000
19Utalii (Tourism)Miezi 3176,000
20Utunzaji Kumbukumbu (Records Management and Filing)Miezi 6336,000
21Unyooshaji wa Bodi za Magari (Auto Body Repair)Miezi 6406,000
22Ukerezaji Vyuma (Fitter Mechanics)Miezi 6386,000
23Matengenezo ya Kompyuta (Computer Maintenance)Wiki 22385,000
24Uhudumu wa Ofisi (Office Attendant)Miezi 3261,000
25Masomo Mbebezi (Related Subject) – Level IIMiezi 9258,000
26Masomo Mbebezi (Related Subject) – Level IIIMiezi 6186,000

Jinsi ya Kutuma Maombi ya Kujiunga na VETA Tanga 2026

Wanafunzi wanaotaka kujiunga na Chuo cha Ufundi Stadi Tanga wanaweza kuanza mchakato wa maombi kwa kutumia mfumo wa VETA. Fuata hatua hizi:

  1. Tembelea tovuti ya maombi ya VETA
  2. Tafuta sehemu ya maombi ya kujiunga na vyuo vya VETA.
  3. Chagua Chuo cha Ufundi Stadi Tanga.
  4. Angalia kozi zinazopatikana na taarifa zake.
  5. Fuata maelekezo ya mfumo ili kukamilisha maombi.

Ni vizuri kuwasiliana na chuo ili kuthibitisha upatikanaji wa kozi, ada na masharti ya kujiunga kabla ya kufanya malipo.

Mawasiliano ya Chuo cha VETA Tanga

Kwa maelezo zaidi kuhusu kozi, muda wa mafunzo, ada na udahili, unaweza kuwasiliana na chuo kupitia taarifa zifuatazo:

  • Jina la Chuo: Chuo cha Ufundi Stadi Tanga (Tanga RVTSC)
  • Anwani: S.L.P. 1204, Tanga, Tanzania
  • Simu: 027 264 4617 / 027 264 4271
  • Nukushi: 027 264 4272
  • Barua Pepe: tangarvtsc@veta.go.tz

Hitimisho

Chuo cha VETA Tanga kinatoa kozi 26 katika fani mbalimbali, zikiwemo udereva, ufundi wa magari, umeme, kompyuta, ujenzi, upishi na utalii. Wanafunzi wanaotaka kupata ujuzi wa ufundi stadi wanaweza kuchagua kozi inayolingana na malengo yao na kuwasiliana na chuo kwa maelezo zaidi kuhusu udahili na ada.

Soma zaidi: Matokeo ya Darasa la Saba 2026 NECTA Shule Zote Dodoma