Fahamu orodha ya kozi za VETA Tanga 2026, muda wa mafunzo na ada zake kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi. Chuo cha Ufundi Stadi Tanga (Tanga RVTSC) kinatoa kozi mbalimbali zinazohusiana na udereva, ufundi wa magari, umeme, kompyuta, ujenzi, upishi, utalii na fani nyingine.
Bonyeza hapa kutuma maombi Chuo cha VETA Tanga 2026
Wanafunzi wanaweza kuchagua kozi kulingana na malengo yao ya kujifunza ujuzi wa kazi na kujiajiri au kuajiriwa.
Orodha ya Kozi za VETA Tanga 2026 na Ada Zake
Chuo cha VETA Tanga kinatoa kozi zenye muda tofauti wa mafunzo na ada kulingana na fani. Jedwali lifuatalo linaonyesha orodha ya kozi, muda wa mafunzo na ada zilizotolewa.
| Na. | Jina la Kozi | Muda wa Mafunzo | Ada (TSh) |
|---|---|---|---|
| 1 | Udereva wa Awali (Basic Driving of Motor Vehicle) | Wiki 5 | 232,000 |
| 2 | Udereva wa Magari ya Abiria (PSV) | Wiki 2 | 235,000 |
| 3 | Ufundi wa Magari (Motor Vehicle Mechanics) | Miezi 6 | 386,000 |
| 4 | Ufundi Umeme (Electrical Installation) | Miezi 6 | 386,000 |
| 5 | Useremala (Carpentry and Joinery) | Miezi 6 | 316,000 |
| 6 | Ufundi wa Umeme wa Magari (Auto-Electricity) | Miezi 6 | 386,000 |
| 7 | Upakaji Rangi na Uchoraji (Painting and Sign Writing) | Miezi 6 | 316,000 |
| 8 | Uhazili (Computer and Secretarial) | Miezi 6 | 351,000 |
| 9 | Ushonaji (Designing, Sewing and Cloth Technology) | Miezi 3 | 286,000 |
| 10 | Matumizi ya Kompyuta (Computer Application – Programu Saba) | Miezi 3 | 305,000 |
| 11 | Uchomeleaji Vyuma (Welding and Metal Fabrication) | Miezi 6 | 336,000 |
| 12 | Ufundi Bomba (Plumbing and Drainage) | Miezi 6 | 336,000 |
| 13 | Ufundi Uashi (Masonry and Brick Laying) | Miezi 6 | 316,000 |
| 14 | Utunzaji wa Vyumba/Nyumba (Housekeeping) | Miezi 3 | 306,000 |
| 15 | Mapokezi ya Wageni na Kompyuta (Front Office Operation and CA) | Miezi 3 | 378,000 |
| 16 | Mapishi (Food Production) | Miezi 3 | 296,000 |
| 17 | Huduma za Vyakula na Vinywaji (Food and Beverage Services) | Miezi 3 | 316,000 |
| 18 | Uokaji na Ukaangaji (Basic Bakery and Pastry Production) | Miezi 3 | 406,000 |
| 19 | Utalii (Tourism) | Miezi 3 | 176,000 |
| 20 | Utunzaji Kumbukumbu (Records Management and Filing) | Miezi 6 | 336,000 |
| 21 | Unyooshaji wa Bodi za Magari (Auto Body Repair) | Miezi 6 | 406,000 |
| 22 | Ukerezaji Vyuma (Fitter Mechanics) | Miezi 6 | 386,000 |
| 23 | Matengenezo ya Kompyuta (Computer Maintenance) | Wiki 22 | 385,000 |
| 24 | Uhudumu wa Ofisi (Office Attendant) | Miezi 3 | 261,000 |
| 25 | Masomo Mbebezi (Related Subject) – Level II | Miezi 9 | 258,000 |
| 26 | Masomo Mbebezi (Related Subject) – Level III | Miezi 6 | 186,000 |
Jinsi ya Kutuma Maombi ya Kujiunga na VETA Tanga 2026
Wanafunzi wanaotaka kujiunga na Chuo cha Ufundi Stadi Tanga wanaweza kuanza mchakato wa maombi kwa kutumia mfumo wa VETA. Fuata hatua hizi:
- Tembelea tovuti ya maombi ya VETA
- Tafuta sehemu ya maombi ya kujiunga na vyuo vya VETA.
- Chagua Chuo cha Ufundi Stadi Tanga.
- Angalia kozi zinazopatikana na taarifa zake.
- Fuata maelekezo ya mfumo ili kukamilisha maombi.
Ni vizuri kuwasiliana na chuo ili kuthibitisha upatikanaji wa kozi, ada na masharti ya kujiunga kabla ya kufanya malipo.
Mawasiliano ya Chuo cha VETA Tanga
Kwa maelezo zaidi kuhusu kozi, muda wa mafunzo, ada na udahili, unaweza kuwasiliana na chuo kupitia taarifa zifuatazo:
- Jina la Chuo: Chuo cha Ufundi Stadi Tanga (Tanga RVTSC)
- Anwani: S.L.P. 1204, Tanga, Tanzania
- Simu: 027 264 4617 / 027 264 4271
- Nukushi: 027 264 4272
- Barua Pepe: tangarvtsc@veta.go.tz
Hitimisho
Chuo cha VETA Tanga kinatoa kozi 26 katika fani mbalimbali, zikiwemo udereva, ufundi wa magari, umeme, kompyuta, ujenzi, upishi na utalii. Wanafunzi wanaotaka kupata ujuzi wa ufundi stadi wanaweza kuchagua kozi inayolingana na malengo yao na kuwasiliana na chuo kwa maelezo zaidi kuhusu udahili na ada.
Soma zaidi: Matokeo ya Darasa la Saba 2026 NECTA Shule Zote Dodoma




Leave a Reply
View Comments