Ukinunua umeme wa LUKU lakini token hazijafika kwenye simu yako, au umefuta ujumbe wenye token kabla ya kuingiza kwenye mita, usiwe na wasiwasi. Token zako hazijapotea, unaweza kuzipata tena kwa kutumia njia mbalimbali za huduma za TANESCO na GePG.
Bonyeza hapa kupata token za LUKU Tanesco
Kuna njia tatu rahisi za kupata token za umeme ulizonunua, ambazo ni kupitia Twiga Chatbot kwenye tovuti ya TANESCO, USSD kwa kupiga 15200# na kutumia GePG App.
Njia ya 1: Kupata Token za LUKU Kupitia Twiga Chatbot
Unaweza kupata token zako za mwisho ulizonunua kupitia tovuti rasmi ya TANESCO kwa kufuata hatua hizi:
- Tembelea tovuti rasmi ya TANESCO
- Chagua sehemu ya Huduma ya Mita.
- Chagua Pata Token Uliyonunua.
- Ingiza namba ya mita yako.
- Bofya OK ili kuendelea.
Baada ya kukamilisha hatua hizo, utaweza kuona token zako za mwisho ulizonunua na kuzipata tena kwa ajili ya kuingiza kwenye mita yako ya umeme.
Njia ya 2: Kupata Token za LUKU kwa Kupiga *152*00#
Njia nyingine ya kupata token za umeme zilizopotea ni kutumia huduma ya USSD kupitia simu yako. Fuata hatua hizi:
- Piga *152*00# kwenye simu yako.
- Chagua 4 – Nishati, Madini na Usafiri.
- Chagua 4 – TANESCO.
- Chagua 4 – Angalia Token za Umeme.
- Ingiza namba ya mita yako.
- Bofya OK au fuata maelekezo yanayoonekana kwenye simu yako.
Baada ya hapo, mfumo utakusaidia kupata token zako za mwisho za umeme ulizonunua.
Njia ya 3: Kupata Token za LUKU Kupitia GePG App
Unaweza pia kutumia programu ya GePG kupata token za umeme ulizonunua kwa kufuata hatua hizi:
- Pakua programu ya GePG kupitia Google Play Store au Apple App Store.
- Fungua programu na uchague LUKU.
- Chagua Last Token (Umeme wa Mwisho).
- Tafuta token kwa kutumia mojawapo ya taarifa zifuatazo:
- Namba ya simu uliyotumia kununua umeme.
- Namba ya mita.
- GePG Reference Number.
- Namba ya risiti.
- Ingiza taarifa husika.
- Bofya Search.
Mfumo utaonyesha taarifa za token yako ya mwisho, ikiwemo token, tarehe ya manunuzi na kiasi cha fedha ulicholipia.
Hitimisho
Token za LUKU zikichelewa kufika au ukifuta ujumbe wa token ulizonunua, si lazima ununue umeme tena. Unaweza kuzirejesha kwa kutumia tovuti ya TANESCO, huduma ya USSD *152*00# au GePG App.
Hakikisha unatumia namba sahihi ya mita au taarifa ulizotumia wakati wa kununua umeme ili kurahisisha upatikanaji wa token zako.
Soma zaidi: Kozi za VETA Rukwa 2026: Muda na Ada




Leave a Reply
View Comments