Fahamu orodha ya kozi za VETA Mbarali 2026, muda wa mafunzo na ada zake. Chuo cha Ufundi Stadi Mbarali (Mbarali DVTC), kilichopo Rujewa, kinatoa mafunzo ya ufundi stadi katika fani mbalimbali zinazowawezesha wanafunzi kupata ujuzi wa vitendo kwa ajili ya kujiajiri au kuajiriwa.
Bonyeza hapa kutuma maombi ya VETA Mbarali 2026
Kozi zinazotolewa chuoni hapo zinahusisha udereva, ufundi umeme, ufundi magari, ushonaji, matumizi ya kompyuta, uashi, uchomeleaji vyuma, urembo na ususi pamoja na upishi.
Orodha ya Kozi za VETA Mbarali 2026
Hapa chini ni orodha ya kozi zinazotolewa katika Chuo cha Ufundi Stadi Mbarali, muda wa mafunzo na ada kwa kila kozi.
| Na. | Jina la Kozi | Muda wa Mafunzo | Ada (TSh) |
|---|---|---|---|
| 1 | Udereva wa Awali (Basic Motor Driving Course) | Wiki 5 | 200,000 |
| 2 | Udereva wa Pikipiki na Bajaji (Basic Motorcycle Driving) | Wiki 2 | 70,000 |
| 3 | Ufundi Umeme | Miezi 3 | 200,000 |
| 4 | Ufundi Magari (Basic Motor Vehicle Mechanics) | Miezi 3 | 200,000 |
| 5 | Ufundi wa Awali wa Ushonaji (Basic Sewing and Cloth Technology) | Miezi 3 | 200,000 |
| 6 | Matumizi ya Kompyuta (Basic Computer Applications) | Miezi 3 | 150,000 |
| 7 | Ufundi Uashi (Masonry and Bricklaying) | Miezi 3 | 200,000 |
| 8 | Uungaji Vyuma (Basic Welding and Metal Fabrication) | Miezi 3 | 200,000 |
| 9 | Urembo na Ususi (Salon and Hair Dressing) | Miezi 3 | 200,000 |
| 10 | Upishi (Food Production) | Miezi 3 | 200,000 |
Jinsi ya Kutuma Maombi ya Kujiunga na VETA Mbarali
Waombaji wanaotaka kujiunga na Chuo cha Ufundi Stadi Mbarali wanaweza kutuma maombi kupitia mfumo rasmi wa VETA kwa kutumia kiungo kifuatacho:
Unashauriwa kufuata maelekezo yaliyopo kwenye mfumo na kuchagua kozi unayotaka kusomea.
Mawasiliano ya Chuo cha VETA Mbarali
Kwa maelezo zaidi kuhusu kozi zinazotolewa, ada, udahili na masharti ya kujiunga, unaweza kuwasiliana na chuo kupitia mawasiliano yafuatayo:
- Jina la Chuo: Chuo cha Ufundi Stadi Mbarali
- Anuani: S.L.P. 62, Rujewa, Tanzania
- Simu: +255 712 350 039
- Barua pepe: mbaralidvtc@veta.go.tz
Hitimisho
VETA Mbarali inatoa fursa ya kupata ujuzi katika fani mbalimbali za ufundi stadi. Waombaji wanaweza kuchagua kozi kulingana na malengo yao, muda wa mafunzo na uwezo wa kulipa ada. Kwa taarifa zaidi kuhusu udahili, wasiliana na Chuo cha Ufundi Stadi Mbarali kupitia mawasiliano yaliyotolewa hapo juu.
Soma zaidi: Kozi za VETA Ikungi 2026: Muda na Ada




Leave a Reply
View Comments