Muhtasari wa Matokeo ya Kidato cha Sita 2026 NECTA Huu Hapa

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa waliochaguliwa kidato cha tano 2026, Matokeo ya kidato cha sita 2026 kujiunga na vyuo, nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Muhtasari wa Matokeo ya Kidato cha Sita 2026 NECTA Huu Hapa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Mkutano wake wa 172 uliofanyika tarehe 4 Julai 2026 katika ofisi zake za Mikocheni, Dar es Salaam, liliidhinisha kutangazwa rasmi kwa matokeo ya mitihani iliyofanyika mwezi Mei 2026.

Mitihani Iliyotangazwa

NECTA ilitangaza matokeo ya mitihani ifuatayo:

1. Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE)

Mtihani wa Advanced Certificate of Secondary Education Examination (ACSEE) kwa watahiniwa wa shule na kujitegemea.

2. Mitihani ya Ualimu kwa Mitaala ya Zamani

  • Grade A Teacher’s Certificate Examination (GATCE)
  • Diploma in Secondary Education Examination (DSEE)

3. Mitihani ya Ualimu kwa Mitaala Iliyoboreshwa ya 2023

  • Diploma in Primary Education Examination (DPEE)
  • Diploma in Pre-Primary Education Examination (DPPEE)
  • Diploma in Special Education Examination (DSPEE)

Takwimu za Usajili wa ACSEE 2026

Jumla ya watahiniwa 133,647 walijiandikisha kufanya mtihani wa Kidato cha Sita.

  • Wanawake: 65,217 (48.80%)
  • Wanaume: 68,430 (51.20%)

Kati yao:

  • Watahiniwa wa shule: 126,556
  • Watahiniwa wa kujitegemea: 7,091

Mahudhurio ya Watahiniwa wa Shule

Kati ya watahiniwa wa shule:

  • Waliofanya mtihani: 125,320 (99.02%)
  • Hawakufanya mtihani: 1,236 (0.98%)

Kwa jinsia:

  • Wanawake waliofanya mtihani: 61,835 (99.12%)
  • Wanaume waliofanya mtihani: 63,485 (98.93%)

Mahudhurio ya Watahiniwa wa Kujitegemea

Kati ya watahiniwa 7,091 waliosajiliwa:

  • Waliofanya mtihani: 6,476 (91.33%)
  • Hawakufanya mtihani: 615 (8.67%)

Takwimu za Mitihani ya Ualimu

GATCE

  • Waliosajiliwa: 4
  • Waliofanya mtihani: 4

DSEE

  • Waliosajiliwa: 1,540
  • Waliofanya mtihani: 1,523 (98.90%)
  • Hawakufanya mtihani: 17 (1.10%)

DPEE

  • Waliosajiliwa: 10,672
  • Waliofanya mtihani: 10,427
  • Hawakufanya mtihani: 245 (2.30%)

Kwa jinsia:

  • Wanawake waliofanya mtihani: 6,720 (98.20%)
  • Wanaume waliofanya mtihani: 3,707 (96.81%)

Soma zaidi: NECTA Matokeo ya Mtihani wa Ualimu 2026 DSEE, GATCE, DPEE, DPPEE na DSPEE