Programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT) Nkasi 2026 | Fursa kwa Vijana na Wanawake

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa waliochaguliwa kidato cha tano 2026, Matokeo ya kidato cha sita 2026 kujiunga na vyuo, nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi imetangaza nafasi za kujiunga na Programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT) kwa vijana na wanawake kupitia kilimo cha shamba la pamoja. Tuma maombi kuanzia 1–14 Septemba 2026.

Tangazo la Programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT) 2026

Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa inawatangazia vijana na wanawake wenye sifa stahiki kuomba kujiunga na Programu ya Jenga Kesho Iliyobora (Building Better Tomorrow – BBT) kupitia kilimo cha shamba la pamoja katika Vijiji vya Mwenge na Kate, Kata ya Kate.

Lengo la programu ni kuwawezesha vijana na wanawake kuongeza uzalishaji wa kilimo, kujiajiri na kuwa mfano wa maendeleo ya kilimo katika jamii.

Sifa na Vigezo vya Kujiunga

Waombaji wanapaswa kutimiza masharti yafuatayo:

  • Awe Mtanzania na mkazi wa Wilaya ya Nkasi.
  • Kijana awe na umri wa miaka 18–40.
  • Mwanamke awe na umri usiozidi miaka 65 na mwenye nguvu za kufanya kazi.
  • Awe anajua kusoma na kuandika.
  • Awe na tabia njema, mwaminifu na mchapakazi.
  • Awe na afya njema ya kushiriki kikamilifu katika programu.
  • Awe tayari kusaini na kuzingatia masharti ya mradi.
  • Awe anajishughulisha na kilimo na kumiliki ardhi kati ya ekari 1–10.
  • Awe tayari kuwa mfano kwa vijana na wanawake wengine.
  • Asiwe ameajiriwa katika Serikali, sekta binafsi au taasisi nyingine rasmi.

Kipaumbele kitapewa vijana na wanawake wanaotoka katika eneo la mradi (Mwenge na Kate).

Nyaraka Zinazotakiwa

Maombi yaambatanishwe na:

  1. Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA.
  2. Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Kijiji au Mtaa inayoonyesha ushiriki wa mwombaji katika shughuli za kilimo.
  3. Nyaraka nyingine muhimu zitakazothibitisha sifa za mwombaji.

Jinsi ya Kuwasilisha Maombi

Maombi yote yanapaswa kupitishwa na Mtendaji wa Kijiji au Kata husika kisha kuwasilishwa katika Ofisi ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.

Muda wa kupokea maombi: 1 Septemba – 14 Septemba 2026

Anuani ya kuwasilisha maombi:

Mkurugenzi Mtendaji (W), Nkasi Barabara ya Ikulu S.L.P. 02 Namanyere, Nkasi – Rukwa

Ratiba Muhimu

TukioTarehe
Kuanza kupokea maombi1 Septemba 2026
Mwisho wa kupokea maombi14 Septemba 2026
Eneo la mradiMwenge na Kate, Nkasi

Hitimisho

Programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT) 2026 ni fursa kwa vijana na wanawake wa Wilaya ya Nkasi wanaojishughulisha na kilimo na wanaotaka kuimarisha uzalishaji kupitia shamba la pamoja. Hakikisha unakamilisha nyaraka zote na kuwasilisha maombi yako kabla ya 14 Septemba 2026.

Soma zaidi: Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Ghala Kuu la Korosho 2026/2027 WRRB