Sifa za Kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa Kujitolea 2026 na Vifaa vya Kuripoti Navyo Kambini

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa waliochaguliwa kidato cha tano 2026, Matokeo ya kidato cha sita 2026 kujiunga na vyuo, nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Vijana wanaotarajia kujiunga na Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa Kujitolea mwaka 2026 wanapaswa kutimiza sifa zilizowekwa na Jeshi hilo. Sifa hizo zinahusisha uraia, umri, kiwango cha elimu, afya na tabia ya mwombaji. Pia, vijana watakaochaguliwa wanatakiwa kuripoti kambini wakiwa na vifaa maalumu kwa ajili ya mafunzo.

Bonyeza hapa kuona sifa na maelekezo ya kujiunga na JKT

Katika makala hii, tumeeleza sifa za waombaji kulingana na kiwango chao cha elimu pamoja na orodha ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo baada ya kuandikishwa.

Sifa za Muombaji wa Mafunzo ya JKT kwa Kujitolea 2026

Mwombaji wa mafunzo ya JKT kwa Kujitolea anatakiwa kutimiza masharti yafuatayo:

  1. Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
  2. Awe na umri unaokubalika kulingana na kiwango chake cha elimu kama ifuatavyo:

Umri na Sifa za Elimu kwa Waombaji

a. Vijana wenye Elimu ya Msingi (Darasa la Saba)

  • Umri uwe kuanzia miaka 16 hadi 18.
  • Awe amemaliza Elimu ya Msingi mwaka 2023, 2024, 2025 au 2026.
  • Awe na cheti halisi cha kumaliza Elimu ya Msingi.

b. Vijana wenye Elimu ya Sekondari (Kidato cha Nne)

  • Umri usiwe zaidi ya miaka 20.
  • Awe amemaliza Elimu ya Sekondari mwaka 2022, 2023, 2024 au 2025.
  • Awe na cheti halisi cha kumaliza Elimu ya Sekondari (Secondary Leaving Certificate) na cheti halisi cha matokeo (Academic Certificate).
  • Awe na ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Nne.
  • Mwombaji mwenye Daraja la Nne anatakiwa kuwa na alama kuanzia 26 hadi 32.
  • Awe pia na cheti halisi cha kumaliza Elimu ya Msingi.

c. Vijana wenye Elimu ya Kidato cha Sita

  • Umri usiwe zaidi ya miaka 22.
  • Awe amemaliza Elimu ya Sekondari mwaka 2022, 2023, 2024 au 2025.
  • Awe na cheti halisi cha kumaliza Elimu ya Sekondari (Secondary Leaving Certificate) na cheti halisi cha matokeo (Academic Certificate).
  • Awe na ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Nne.
  • Awe na cheti halisi cha kumaliza Elimu ya Msingi.

d. Vijana wenye Elimu ya Stashahada (Diploma)

  • Umri usiwe zaidi ya miaka 25.
  • Awe na vyeti vya Elimu ya Msingi na Sekondari.
  • Awe na cheti cha chuo au cheti cha matokeo ya masomo ya chuo.

e. Vijana wenye Elimu ya Shahada (Degree)

  • Umri usiwe zaidi ya miaka 26.
  • Awe na vyeti vya Elimu ya Msingi na Sekondari.
  • Awe na cheti cha chuo au cheti cha matokeo ya masomo ya chuo.

f. Vijana wenye Elimu ya Shahada ya Uzamili (Master’s Degree)

  • Umri usiwe zaidi ya miaka 27.
  • Awe na vyeti vya Elimu ya Msingi na Sekondari.
  • Awe na cheti cha chuo au cheti cha matokeo ya masomo ya chuo.

Masharti Mengine ya Mwombaji

Mbali na sifa za umri na elimu, mwombaji anatakiwa:

  1. Awe na afya njema na akili timamu, na asiwe na alama za michoro mwilini (tattoo).
  2. Awe na tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia mahakamani na hajawahi kufungwa.
  3. Awe na Kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
  4. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate).
  5. Asiwe amewahi kutumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo, wala kuajiriwa katika idara nyingine za Serikali.
  6. Asiwe amewahi kupitia mafunzo ya JKT katika operesheni zilizopita, kwa kundi la kujitolea au kundi la lazima (Mujibu wa Sheria).
  7. Asiwe anajihusisha au amewahi kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya, bangi na vitu vingine vinavyofanana na hivyo.

Angalizo: Kijana atakayebainika kuwa na nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua kali za kisheria kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

Vifaa vya Kuripoti Navyo Kambini JKT 2026

Baada ya kuandikishwa na kupangiwa kwenda kambini, vijana wanatakiwa kujiandaa na vifaa vifuatavyo:

  1. Bukta ya rangi ya Dark Blue: Iwe na mpira kiunoni (elastic), mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini na isiwe na zipu. Kwa vijana wa kike, bukta iwe na mpira kiunoni na kwenye pindo za miguu.
  2. Raba za michezo: Zenye rangi ya kijani au bluu.
  3. Mashuka mawili: Ya kulalia yenye rangi ya bluu bahari.
  4. Soksi: Ndefu zenye rangi nyeusi.
  5. Nguo za kuzuia baridi: Kwa vijana watakaopangiwa mikoa yenye baridi.
  6. Truck suit: Yenye rangi ya kijani au bluu.
  7. Flana: Ya rangi ya kijani kibichi, yenye kola ya duara na isiyo na maandishi.
  8. Chandarua: Chenye rangi ya kijani au bluu.

Hitimisho

Vijana wanaotarajia kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa Kujitolea 2026 wanashauriwa kuhakikisha wanatimiza masharti yote ya elimu, umri, afya na nidhamu kabla ya kuripoti kambini. Pia, ni muhimu kuandaa vifaa vilivyotajwa mapema ili kuepuka usumbufu wakati wa kuanza mafunzo.

Mwombaji anapaswa kuhakikisha vyeti na nyaraka zake ni halisi, kwa kuwa matumizi ya nyaraka za kughushi yanaweza kusababisha kuchukuliwa hatua za kisheria.

Soma zaidi: JKT Kujitolea 2026/27: Tangazo la Kujiunga na Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa